44 – al-Khuraybiy (126-213), mmoja katika maimamu wa masimulizi

191 – ´Aliy bin Abiyr-Rabiy´ al-Bazzaar amesema:

”Nilimwendea Bishr bin al-Haarith na kusema: ”Ee Abu Naswr! Umesikia chochote kuhusu Qur-aan?” Akasema: ”Nilimuuliza ´Abdullaah bin Daawuud al-Khuraybiy kuhusu hilo, kisha akanisomea mwisho wa ”al-Hashr”:

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ

”Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye.”[1]

Kisha akasema: ”Je, hili ni kiumbe?” Ulinzi unaombwa kwa Allaah!”[2]

192 – ´Abdullaah bin Muhammad bin Asmaa’ amesimulia kwamba al-Khuraybiy amesema:

”Wakati nilipokuwa natembea Abadan na nikawa naihadithia nafsi yangu juu ya uumbwaji wa Qur-aan, mtu mmoja akanishika kwa nyuma yangu, akanitikisa na kusema: ”Ee mwana wa Daawuud, kuwa imara! Hakika maneno ya Allaah si kiumbe.” Nikageuka na simuona yeyote.”[3]

[1] 59:23

[2] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu.

[3] Ibn Asmaa´ ni madhubuti, mtukufu na ni miongoni mwa wasimulizi wa al-Bukhaariy na Muslim. Ikiwa cheni ya wapokezi imesihi hadi kwake, basi masimulizi nayo ni Swahiyh. Hata hivyo sijapata chochote juu yake hadi sasa.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 160-161
  • Imechapishwa: 12/01/2025
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy