3 – Sa´d bin Abiy Waqqaas amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Safisheni nyua zenu na wala msijifananishe na mayahudi. Wanakusanya taka katika nyumba zao.”[1]

[1] Hadiyth ni nzuri. Ameipokea ad-Duulaabiy katika ”al-Kunaa” (2/137) kupitia kwa Abut-Twayyib Haarun bin Muhammad: Bukayr bin Sammaar ametuhadithia, kutoka kwa ´Aamir bin Sa´d, kutoka kwa Sa´d aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah ni msafi na anapenda usafi, mwenye kutoa na anapenda kutoa, mkarimu na anapenda ukarimu, mzuri na anapenda vizuri… ”

Wapokezi wake ni wenye kuaminika, isipokuwa Abut-Twayyib Haarun bin Muhammad, ambaye ni mnyonge mno. Hata hivyo ameipokea at-Tirmidhiy kupitia njia nyingine; kutoka kwa Khaalid bin Ilyaas, kutoka kwa Swaalih bin Abiy Hassaan: Nimemsikia Sa´iyd bin al-Musayyab akisema… Akataja Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akasema: ”Nikamtajia hayo Muhaajir bin Mismaar ambaye alisema: ”´Aamir bin Sa´d amenihadithia mfano wa hayo, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

at-Tirmidhiy amesema:

”Hadiyth ni geni. Khaalid bin Ilyaas ni mnyonge.”

Ni kweli, lakini inaweza kutiwa nguvu na ile njia ya kwanza. Kinachozidi kuitia nguvu ni yale aliyosimulia Sa´d kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Safisheni nyua zenu. Kwani hakika mayahudi hawasafishi nyua zao.”

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw”. Mshereheshaji al-Munaawiy amesema:

”al-Haythamiy amesema kuwa wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh isipokuwa tu mwalimu wa at-Twabaraaniy.”

Kwa kukata kabisa njia hii sio zile mbili za mwanzo. Kwa hivyo ushahidi wenye nguvu kabisa wa lengo la Hadiyth – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

Kisha nikapata cheni ya wapokezi ya at-Twabaraaniy katika ”Zawaa’id-ul-Mu´jam as-Swaghiyr al-Awsatw” (02/11) na nikaona mambo ni kama alivosema al-Haythamiy. Isipokuwa tu mwalimu wa at-Twabaraaniy ambaye ni ´Aliy bin Sa´iyd ar-Raaziy ambaye kuna maoni mbalimbali juu yake. Maoni yenye nguvu ni kwamba Hadiyth zake ni nzuri pale anapokuwa hakupingana na wengine.

Isitoshe Hadiyth ina upokezi mwingine wenye kuitia nguvu lakini ambao kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi. Ameipokea Wakiy´ bin al-Jarraah katika ”az-Zuhd” kwa cheni ya wapokezi dhaifu. Kwa ujumla ni kwamba Hadiyth imethibiti kabisa kutokana na njia hizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 197-198
  • Imechapishwa: 21/11/2023