Ibn Jurayj ametamka wazi amehadithia kutoka kwa nani kwa ´Abdur-Razzaaq, kama ilivyo katika ”al-Ahkaam” ya ´Abdul-Haqq al-Ishbiyliy. Halafu nikaiona kwa ”al-Muswannaf” (2/198) ya ´Abdur-Razzaaq. Kwa hivyo ikaondoka kasoro na Hadiyth ikawa Swahiyh. ´Abdur-Razzaaq amesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekaripia mtu kuuegemea mkono wake wa kushoto anapokuwa anakula.”[1]

Wapokezi wake ni wenye kuaminika, lakini kunakosekana wasimulizi kadhaa mfululizo katika cheni yake ya wapokezi. Hata hivyo inatiliwa nguvu na yenye kuenea yaliyotangulia – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Vilevile inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ´Umar:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona bwana mmoja ameuegemea mkono wake wa kushoto ambapo akasema: ”Usiketi namna hiyo. Huo ni mkao wa wale wanaoadhibiwa.”

Ameipokea Ahmad (5972) kwa cheni ya wapokezi nzuri na Swahiyh.

[1] al-Muswannaf (10/415).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 196-197
  • Imechapishwa: 21/11/2023