4 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jihadharani na kete mbili zilizowekwa alama zikitupwa huku na huku. Ni kamari ya wasiokuwa waarabu.”[1]

[1] Ahmad (4263) na al-Bayhaqiy kupitia kwa Ibraahiym bin Muslim al-Hijriy, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa Ibn Mas´uud. al-Hijriy alikuwa dhaifu. Amesimulia Athar hiyo kutoka kwa Ibn Mas´uud. al-Bayhaqiy pia ameipokea na akasema:

”Ni yenye kuhifadhiwa.”

Udhahiri ni kuwa imepokelewa kupitia njia nyingine isiyokuwa ya al-Hijriy. al-Haythamiy ameitaja na kusema:

”Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy. Wanaume wa at-Twabaraaniy ni wanaume wa Swahiyh.” (Majma´-uz-Zawaa’id (8/113))

al-Hijriy sio katika wanaume wa Swahiyh, jambo linalojulisha kuwa at-Twabaraaniy ameipokea kupitia njia nyingine. Kwa hivyo Hadiyth inatiwa nguvu nayo, khaswa kwa kuzingatia kuwa kuna njia nyingine inayoitia nguvu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 198-199
  • Imechapishwa: 21/11/2023