14. Mamlaka inaanguka kwa ukafiri na kuritadi

Kuritadi kunapelekea katika hukumu zinazohusiana na hapa duniani na Aakhirah. Miongoni mwa hukumu za kidunia ni pamoja na zifuatazo:

1- Mamlaka inaanguka. Haifai kwa mwenye kuritadi kusimamia kitu ambacho kukisimamia kwake kumeshurutishwa Uislamu. Kujengea juu ya haya mwenye kuritadi hana mamlaka juu ya watoto wake wachanga na wengineo. Haifai kwake kuwaozesha ndugu wanawake kama wasichana wake na wengineo. Wanachuoni wetu (Rahimahum Allaah) wamesema waziwazi katika vitabu vyao ya kwamba imeshurutishwa kwa walii awe ni muislamu ili kumuozesha mwanamke wa Kiislamu. Wamesema vilevile kwamba kafiri hana mamlaka juu ya mwanamke muislamu. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii mwerevu.”

Werevu mkubwa kabisa ni Uislamu na upambavu duni kabisa ni ukafiri na kuritadi kutoka katika Uislamu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ

“Na nani atakayejitenga na dini ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu?”[1]

[1] 02:130

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 17
  • Imechapishwa: 22/10/2016