14. Hadiyth “Je, nisikujuzeni juu ya kitu… “

310 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ألا أدلّكم على ما يمحو الله به الخَطايا، ويرفعُ به الدَّرجات؟

قالوا: بلى يا رسول الله! قال:”  إسباغُ الوضوء على المكاره، وكَثرةُ الخُطا إلى المساجد، وانتظارُ الصلاةِ بعد الصلاةِ، فذلِكم الرباطُ، فذلِكم الرباطُ، فذلِكم الرباطُ

“Je, nisikujuzeni juu ya kitu ambacho Allaah kwacho anafuta makosa na ananyanyua daraja?” Wakaema: “Bila shaka, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Kueneza vizuri wudhuu´ wakati wa machukizo, hatua nyingi kwenda msikitini na kusubiri swalah nyingine baada ya swalah kumalizika.”[1]

Ameipokea Maalik, Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah kwa maana kama hiyo.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/245)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy