13. Hadiyth “Kila kiungo cha mtu kinalazimika kutoa swadaqah… “

309 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

كلُّ سُلامى من الناس عليه صدقةٌ كلَّ يوم تَطلعُ فيه الشمس، تَعدِل بين الاثنين صدقةٌ، وتُعين الرجلَ في دابّته فتحمله أو ترفع له عليها متاعَه صدقةٌ، والكلمةُ الطيبةُ صدقةٌ، وبكل خُطوةٍ يمشيها إلى الصلاة صدقةٌ، وتُميطُ الأذى عن الطريق صدقةٌ

“Kila kiungo cha mtu kinalazimika kutoa swadaqah kwa kila siku inayochomozewa na jua. Kusuluhisha kati ya watu wawili ni swadaqah. Kumsaidia mtu kwenye kipando chake kwa njia ya kwamba ukampandisha juu yake au ukamshushia mizigo yake ni swadaqah. Neno zuri ni swadaqah. Kila hatua anayotembea kwenda msikitini ni swadaqah. Kuodoa chenye kuudhi njiani ni swadaqah.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/244-245)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy