12. Hadiyth “Sikumjua yeyote aliye mbali zaidi na msikiti kuliko yeye… “

308 – Ubayy bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

كان رجلٌ من الأنصارِ لا أعلم أحداً أبعدَ من المسجد منه، كانت لا تُخطِئُهُ صلاةٌ، فقيل له: لو اشتريتَ حماراً تركبه في الظَّلْماء، وفي الرَّمْضاءِ، فقال: ما يَسُرُّني أنَّ منزلي إلى جنْبِ المسجد، إني أريد أن يُكتَبَ لي ممشايَ إلى المسجد، ورجوعي إذا رجعتُ إلى أهلي. فقال رسول الله – صَلَّى اللهُ :عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

“قد جمع الله لك ذلك كلَّه”

“Kulikuwa bwana mmoja katika Answaar, sikumjua yeyote aliye mbali zaidi na msikiti kuliko yeye. Alikuwa hata siku moja haimpiti swalah. Akashauriwa kununua punda wa kumpanda wakati wa giza na wakati wa joto kali, akasema: “Sifurahishwi nyumba yangu iwe karibu na msikiti. Mimi nataka niandikiwe kule kutembelea kwangu kwenda msikitini na kurejea kwangu ninaporudi kwa familia yangu.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah amekukusanyia hayo yote.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

فَتَوَجعْتُ له، فقلت: يا فلان! لو أنك اشتريتَ حماراً يَقيكَ الرَّمْضاء وهوامَّ الأرض؟ قال: أمَا والله ما أحِبُّ أنَّ بيتي مطنَّبٌببيت محمد – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -! قال فَحَملْتُ به حمْلاً  ، حتى أتيتُ نبيَّ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – فأخبرته، فدعاه، فقال له مثل ذلك، وذكر أَنه يرجو أجر الأثر، فقال :النبي – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

“إنَّ لك ما احتَسَبْتَ”

“Nikamuonea huruma na kumwambia: “Ee fulani! Ungelinunua punda anayekukinga na joto na wadudu wa ardhini.” Akasema: “Naapa kwa Allaah! Sipendi nyumba yangu iwe pambizoni na nyumba ya Muhammad (Swalla ´alayhi wa sallam).” Nikachukulia vibaya na nikamwendea Mtume (Swalla ´alayhi wa sallam) na kumweleza jambo hilo. Akamwita na bwana yule akamweleza vivyo hivyo na kwamba anatarajia thawabu za nyayo. Ndipo Mtume (Swalla ´alayhi wa sallam) akasema: “Unapata kile ulichokitarajia.”[1]

Ameipokea Muslim na wengineo. Ibn Maajah amepokea mfano wa upokezi wa pili.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/244)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy