14. Dalili ya kwamba Allaah huweka miguu Yake juu ya al-Kursiy

14- Shu´ayb bin Muhammad bin Ibraahiym ametuhadithia: Haamid bin Muhammad ametuhadithia: Abuu Muslim ametuhadithia: Abuu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan… ح Muhammad bin Muhammad al-Mahmuudiy ametuhadithia: al-Idriys ametuhadithia: Abuu Sa´iyd ametuhadithia: Yahyaa bin Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa Wakiy´, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Ammaar ad-Duhniy, kutoka kwa Muslim al-Butwayn, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“al-Kursiy ni sehemu ya kuwekea miguu na ´Arshi hakuna yeyote awezaye kukadiria kipimo chake.”[1]

Matamshi ni ya al-Wakiy´. Kadhalika imepokelewa kutoka kwa Abuu Muusaa, Abuu Hurayrah, ´Ikrimah na Abuu Maalik[2].

[1] al-Haakim amesema: ”Ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.” (al-Mustadrak (02/282)) na adh-Dhahabiy amesema: ”Wapokezi wake ni waaminifu.” (al-´Uluww, uk. 61) al-Azhariy amesema: ”Usahihi wa upokezi huu wanachuoni wameafikiana nao.” (Tahdhib-ul-Lughah (10(61)).

[2] Tazama ”ad-Durr al-Manthuur” (01/58) na (01/581) ya as-Suyuutwiy.

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 18/01/2017