14. Dalili ya kuwaabudu wasiokuwa Allaah kwa ajili eti ya uombezi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya uombezi ni maneno Yake (Ta´ala):

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”[1]

MAELEZO

Dalili ya madai yao ya kuomba uombezi ni maneno Yake (Ta´ala):

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”

Allaah akawaraddi kwa kusema:

قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ

 “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale asiyoyajua katika mbingu na ardhini?”[2]

Je, nyinyi mnamjuza Allaah juu ya kitu asichokijua mbinguni na ardhini? Yeye (Subhaanah) hatambui kuwa Anaye mshirika katika ´ibaadah. Wao wanathibitisha uombezi na ukaribu. Hata hivyo Allaah akawakufurisha na kuwakadhibisha kwa kitendo hicho.

[1] 10:18

[2] 10:18

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 137
  • Imechapishwa: 05/03/2023