136. Waislamu wanaziachanisha nywele zao katikati

8 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda kuafikiana na watu wa Kitabu katika yale mambo ambayo hakuamrishwa kwayo. Watu wa Kitabu walikuwa wakiziteremsha nywele zao, ilihali washirikiana walikuwa wakiziachanisha kwa kuweka mstari katikati. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa pia akiziteremsha nywele zake kisha baadaye akaziachanisha kwa kuweka msitari katikati.”[1]

[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ahmad. Baadhi wameigemeza kimakosa kwa at-Tirmidhiy, jambo ambalo an-Naabulsiy hakulifanya katika ”adh-Dhakhaa’ir” (3202).

Hadiyth inafahamisha kuwa jambo la mwisho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamua kujitofautisha na washirikina mpaka katika suala la staili ya nywele. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kwa ajili hiyo kuziachanisha nywele kwa kuweka msitari katikati ikawa ni alama ya waislamu, ambapo wale walipa kodi ya kulindwa wakawekewa sharti hiyo kutoachanisha nywele kwa kuweka msitari katikati. Ni kama ambavo Allaah mwanzoni aliweka katika Shari´ah kuelekea Yerusalemu kwa ajili ya kuafikiana na watu wa Kitabu, halafu baadaye akalifuta hilo na akawaamrisha kuielekea Ka´bah:

سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا

”Watasema wapumbavu miongoni mwa watu ´Kipi kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea`?” (2:142) (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 82)

Sababu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuafikiana na watu wa Kitabu pale mwanzoni ni yale aliyosema Haafidhw Ibn Hajar:

”Waabudia mizimu wako mbali zaidi na imani kuliko watu wa Kitabu. Jengine ni kwa sababu watu wa Kitabu wanashikamana na Shari´ah kwa jumla. Kwa ajili hiyo akawa anapenda kuafikiana nao ili awalainishe nyoyo, ingawa kuafikiana nao kulipelekea kwenda kinyume na waabudia mizimu. Wakati waabudia mizimu waliokuwa pamoja naye na waliokuwa wamemgunzuka waliposilimu na watu wa Kitabu wakaendelea kushikilia kufuru yao, akajitofautisha na watu wa Kitabu peke yao.”  (Fath-ul-Baariy)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 192
  • Imechapishwa: 19/11/2023