133. Wenye kuchupa mipaka na wenye kuzembea katika kutangamana na makafiri

Baadhi ya watu wanachukulia wepesi masuala ya kuwapenda waumini kwa ajili ya Allaah na kuwachukia makafiri kwa ajili ya Allaah na wanadai kuwa inahusiana na kutangamana kwa wema, kuudhihirisha Uislamu kwa njia ya kusameheana na kwamba katika Usilamu hakuna mambo ya kuchukiana. Haya ni maneno batili. Uislamu ni dini tukufu, dini yenye nguvu na wala haina kusameheana na makafiri au kuacha kitu cha dini kwa sababu ya makafiri.

Lipo kundi lingine ambalo linawaita waislamu kutowapiga jihaad na vita makafiri. Hoja yao ni kwamba eti Uislamu ni dini ya hurumu na kwamba haina vita.

Kuna kundi lingine ambalo linapetuka mipaka na wanazingatia kwamba kutangamana pamoja na makafiri hakuna maana nyingine isipokuwa ni kuwapenda na wala hawapambanui upambanuzi huu uliotaja Allaah katika Kitabu Chake. Inatakikana kujua mambo haya ya na kuziteremsha hukumu za Shari´ah mahala pake stahiki na wala tusichanganye baina ya haki na batili. Haitakiwi kusema kwamba Uislamu hautakiwi kutangamana na makafiri kwa hali yoyote na wa kwamba ni dini susuwavu na sio dini ya rehema. Katika Uislamu kuna rehema na ususuwavu. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً

”Enyi Mlioamini!  Wapigeni vita wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali.” (at-Tawbah 09:123)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ

”Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka dini yake, basi Allaah atawaleta watu [badala yao] Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya mwenye kulaumu.” (al-Maaidah 05:54)

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao.” (al-Fath 43:29)

Ni wenye huruma kwa waislamu. Lakini kuwa kwao washupavu au wakali kwa makafiri haina maana kwamba hawatangamani nao kabisa katika mambo ambayo Allaah ameruhusu, hawaoi wanawake wa Ahl-ul-Kitaab, hawafanyi nao biashara, si haya yanayokusudiwa. Wanabadilishana na makafiri yale mambo yenye manufaa ambayo wanayahitajia waislamu. Kwa kuwa waislamu wanayahitajia. Ama suala la dini hapana. Katika Dini hakuna mambo ya kulegeza kwa kuacha kitu na wala hakuna kusameheana na dini ya ukafiri kwa kuacha kitu katika Uislamu. Hivyo ni wajibu kuyatambua mambo haya. Kwa sababu masuala haya yamewatatiza wengi katika zama hizi. Wapo ambao wanachukulia wepesi na wanalingania kwamba Uislamu ni ilio salama daima na siku zote. Upande mwingine wanakazia kiasi cha kwamba wanaona kuwa haifai kufanya muamala wowote na makafiri. Makundi yote haya mawili ni yenye kukosea na yanauhujumu Uislamu. Ni wajibu kuyasoma mambo haya na azijue hukumu za Kishari´ah. Kwa sababu huu ni mlango ni muhimu sana na khaswakhaswa katika zama hizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 169-170
  • Imechapishwa: 05/03/2019