132. Masuala yanayohusiana na jinsi ya kutangamana na mzazi kafiri

Suala la sita: Inajuzu kwa waislamu kuwapaka mafuta makafiri. Ikiwa waislamu wataogopa shari ya makafiri, watawapaka mafuta kwa kuepuka shari yao juu ya waislamu. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ

”Waumini hawawafanyi makafiri kuwa marafiki wapenzi wao badala ya waumini na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah.” (Aal ´Imraan 03: 28)

Bi maana atakayejenga urafiki na mapenzi na makafiri kwa kuwapenda na kuwasaidia, Allaah amejitenga naye mbali

إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً

”Isipokuwa mkiwa mnajilinda na shari zao.” (Aal ´Imraan 03: 28)

Bi maana kuwapaka mafuta pindi waislamu watapokhofia wasipatwe na shari yao. Waislamu wanaweza kueipuka shari yao. Si kwa ajili ya kujenga nao urafiki na kuwapenda. Sisi tunawapaka mafuta kwa ajili ya kuiepuka shari yao kwa njia ya kuwapa pesa kwa ajili ya kuepuka shari yao. Yale wanayotaka katika mambo ya kidunia ni kwa ajili ya kuwapaka mafuta ili kuepuka shari yao. Amesema (Ta´ala):

إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً

”Isipokuwa mkiwa mnajilinda na shari zao.”

Tuqaah, Taqiyyah na kupaka mafuta yote yana maana moja. Baadhi ya watu hawatofautishi kati ya mambo hayo na Mudaahanah. Kupaka mafuta inafaa wakati wa dharurah ili kujikinga na shari ya makafiri. Ama Mudaahanah, nako ni kule mtu kuacha kitu katika dini kwa ajili ya kuwaridhisha makafiri, hili ni jambo lisilojuzu kabisa. Haijuzu kufanya Mudaahanah, nako ni kule mtu kuacha kitu katika dini kwa ajili ya kuwaridhisha makafiri. Amesema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ

”Basi usiwatii wanaokadhibisha. Wanatamani lau kama ungelilainisha nao pia walainishe.” (al-Qalam 68:08-09)

Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala) alipokuwa anazumgumzia kuhusu ushukaji wa Qur-aan:

أَفَبِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ

”Je, kwa hadithi hii nyinyi ni wenye kuibeza?” (al-Waaqi´ah 56:81)

Hivi kweli mnaiacha kwa ajili ya kuwaridhisha makafiri? Huku ndio kufanya Mudaahanah.

Kadhalika pindi makafiri walipomuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah wamuabudu Allaah mwaka mmoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) naye aabudu waungu wao mwaka mmoja. Ndipo Alllaah akamkataza juu ya hilo na akateremsha maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَوَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُوَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ  وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ  لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ

”Sema: “Enyi makafiri! Siabudu yale mnayoyaabudu.” Na wala nyinyi si wenye kuabudu Yule ninayemwabudu. Na mimi si mwenye kuabudu yale mnayoabudu. Na wala nyinyi si wenye kuabudu Yule ninayemwabudu – nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu.”(al-Kaafiruun 109:01-06)

Alimkataza kuwakubalia kwa hilo na asilegeze kwa kuacha kitu katika dini ili kuwaridhisha. Haijuzu kulegeza kitu kwa kuacha kitu katika dini ili kuwaridhisha makafiri vovyote hali itavokuwa. Haijuzu kabisa kufanya Mudaahanah. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًإ إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا

”Hakika walikaribia kukukengeusha na yale Tuliyokuletea Wahy ili upate kutuzulia mengineyo. Basi hapo bila shala wangelikufanya rafiki mkubwa. Na lau kama hakukufanya imara, basi hakika ungelikaribia kuelemea kwao kidogo. Hapo bila shaka Tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai na adhabu maradufu [baada ya] kufa, kisha usingelipata mwenye kunusuru dhidi Yetu.” (al-Israa´ 17:73-75)

Haijuzu kulega kwa kuacha kitu katika dini ya Uislamu ili kuwapaka mafuta makafiri Mudaanah haijuzu kabisa. Ama kuwapaka mafuta tu inajuzu wakati wa dharurah. Hii ni ruhusa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً

”Isipokuwa mkiwa mnajilinda na shari zao.” (Aal ´Imraan 03:28)

Ili kujilinda na shari zao. Ni wajibu kuyajua mambo haya. Kwa sababu yanawatatiza watu wengi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 167-169
  • Imechapishwa: 05/03/2019