13. Sababu ya tisa ya talaka ambayo ni kupishana sana kwa miaka

09 – Tofauti kubwa ya umri kati ya wanandoa

Pengine kukawepo tofauti kubwa ya umri kati ya mume na mke, jambo ambalo likawa ni sababu moja wapo ya talaka. Lakini pengine kusitokee talaka, kwa sababu hii sio sababu ya msingi. Hata hivyo pengine ikawa ndio sababu. Si sharti kutofautiana sana kwa miaka iwe ni sababu. Lakini inakuwa ni sababu katika baadhi ya hali. Isingelikuwa nimesikia kwa masikio yangu nisingeifanya kuwa ni sababu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuoa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akiwa na miaka takriban 52 au 53 illihali bibi ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akiwa na miaka 9. Aliishi naye kwa muda wa miaka tisa. Vivyo hivyo Maswahabah walifanya hivo. Lakini nimelitaja hili kwa sababu tuko katika wakati ambao mambo yamebadilika.

Kama nilivyokwelezeni ingelikuwa sijayasikia haya kwa masikio yangu basi nisingelifanya kuwa ni sababu miongoni mwa sababu. Takriban mwezi mmoja uliyopita nimesikia katika kipindi cha ”Nuur ´alaad-Darb” katika majibu ya Muftiy wa Saudi Arabia; Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh mwanamke akiuliza kwa kusema:

”Mimi nimeolewa na umri wangu ni mdogo. Nina watoto wanne ambapo mkubwa wao kafikisha miaka 17. Mume wangu ananizidi zaidi ya miaka 30. Takriban miaka 10 hajaniingilia na mimi nachelea juu ya nafsi yangu na nataka kile wanachokitaka wanawake kutoka kwa waume zao. Je, niombe talaka kutoka kwake?”

Akajibu kwa yale aliyoyajibu kwa kumpa nasaha na akamjuzishia kuomba talaka ikiwa hawezi kusubiri. Kwani hiyo ni haki miongoni mwa haki yake muda wa kuwa hajamwingilia kwa miaka 10.

Kwa kumalizia ni kwamba kupishana sana kwa miaka inaweza kuwa ni sababu miongoni mwa sababu za talaka.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 06/04/2024