Ameona upenyo katika safu ya kwanza bila Sutrah

Swali: Mtu aende katika safu gani anapoona Sutrah katika safu ya pili na katika safu ya kwanza kuna upenyo na hakuna Sutrah?

Jibu: Aswali maeneo pake. Akiwa katika safu ya kwanza aswali katika safu ya kwanza na akiwa katika safu ya pili aswali katika safu ya pili. Sutrah sio jambo la wajibu, ni jambo linalopendeza. Akiwa hachelei kitu na hachelei mtu kupita mbele basi jambo ni lenye wasaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23705/حكم-من-وجد-فرجة-بالصف-الاول-دون-سترة
  • Imechapishwa: 07/04/2024