Muumini hupata raha anaposwali

Swali: Imamu husema:

أرحنا بها

“Tupe raha kwayo.”

badala ya kusema:

“Simamisheni swalah.”?

Jibu: Yamesemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baadhi ya nyakati:

أرحنا بها

“Tupe raha kwayo.”

Kwa maana ya kwamba tupe raha kwa swalah. Kwa msemo mwingine hupata starehe anapoingia ndani ya swalah. Si kwamba awapumzishe nayo. Swalah inampa mtu raha.

أرحنا بها

“Tupe raha kwayo.”

Mwanafunzi: Anapata raha ndani yake?

Ibn Baaz: Muumini anapata starehe ndani yake.

Swali: Aendelee kusema hivo au akemewe?

Jibu: Hapana vibaya. Yamesemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya swalah zake. Amesema:

أرحنا بها يا بلال

“Tupe raha kwayo, ee Bilaal!”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23706/حكم-قول-ارحنا-بها-بدل-اقم-الصلاة
  • Imechapishwa: 07/04/2024