13. Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya makubadhi na soksi za ngozi?

Swali 13: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya makubadhi na soksi za ngozi?

Jibu: Kupangusa juu ya makubadhi haijuzu. Ni lazima kuvua makubadhi na kuosha mguu.

Kuhusu soksi za ngozi ambazo zinafunika mguu, inafaa kufuta juu yake ni mamoja soksi hizo ni za ngozi, pamba, sufu au kitu kingine. Kwa sharti iwe miongoni mwa vile vitu ambavo ni halali kuvitumia. Ama ikiwa ni miongoni mwa vitu ambavo ni haramu kuvaa, kama mfano wa hariri kwa wanamme, ni haramu kupangusa juu yake kwa sababu ni haramu kwake kuivaa. Ikiwa soksi hizo ni halali kwake basi itafaa kufuta juu yake muda wa kuwa amezivaa akiwa na twahara na ni ndani ya ule muda uliopangwa na Shari´ah. Muda uliowekwa ni mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mkazi na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri. Muda huu unaanza kuhesabiwa kuanzia pale mara ya kwanza atakapofuta baada ya kuchengukwa na wudhuu´. Muda huu unaisha masaa ishirini na nne kwa mkazi na masaa sabini na mbili kwa ambaye ni msafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/168)
  • Imechapishwa: 05/05/2021