14. Je, bendeji ina hukumu moja kama soksi za ngozi?

Swali 14: Je, bendeji ina hukumu moja kama soksi za ngozi?

Jibu: Ndio. Ambaye amevaa bendeji ana haki zaidi ya kupewa udhuru kuliko ambaye amevaa soksi za ngozi. Ambaye anavua soksi za ngozi, akaosha mguu kisha akazivaa tena ana wepesi zaidi kuliko yule mwenye kuvaa bendeji kisha akaivaa kwa mara nyingine. Ikiwa Shari´ah imeruhusu kupangusa juu ya soksi za ngozi, basi bendeji itakuwa na haki zaidi ya kufaa. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoagiza kikosi na akawaamrisha kufuta juu ya vijiti na soksi za ngozi. Kutoka kwenye soksi za ngozi tunaweza kufahamu kwamba inafaa kupangusa juu ya bendeji kwa sababu pia zinatia joto na kunapatikana lengo lilelile kama la soksi za ngozi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/168-169)
  • Imechapishwa: 05/05/2021