12. Je, imeshurutishwa ili mtu aweze kupangusa juu ya soksi za ngozi zithibiti zenyewe?

Swali 12: Je, imeshurutishwa ili mtu aweze kupangusa juu ya soksi za ngozi zithibiti zenyewe?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba jambo hilo halikushurutishwa. Dalili zinazojulisha kufuta juu ya soksi za ngozi zimekuja kwa njia ya kuachia. Kizuizi kiko wapi muda wa kuwa zinamnufaisha na anaweza kutembea nazo? Pengine mtu huyu hana isipokuwa soksi za ngozi hizi peke yake. Huenda pia ni mgonjwa na asiyeweza kutikisika na amevaa soksi hizi ili kupata joto kidogo. Kwa hiyo hakuna dalili ya sharti hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/167-168)
  • Imechapishwa: 05/05/2021