11. Ni ipi hukumu ya kupangusa soksi zenye matundu na nyembamba?

Swali 11: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi zenye matundu na nyembamba?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba inafaa kupangusa juu ya soksi zenye matundu na soksi nyembamba ambazo na ambazo ngozi inaonekana kwa nyuma yake. Lengo la kupangusa juu ya soksi na venginevyo sio kule kufunika. Mguu sio kiungo cha siri ambacho ni lazima kukifunika. Lengo ni ruhusa na kumfanyia wepesi mja kwa njia ya kwamba asilazimike kuvua soksi au soksi za ngozi hizi wakati anapotawadha. Bali tunasema kwamba inatosha kufuta juu yake. Hii ndio sababu ikawekwa katika Shari´ah kufuta juu ya soksi za ngozi. Sababu hii kama unavoona mwenyewe inahusu soksi za ngozi, zilizo na matundu, zilizosalimika, nyembamba na soksi nzito.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/167)
  • Imechapishwa: 05/05/2021