13. Ndio maana waislamu wamekuwa wanyonge na makafiri watukufu

”… wala hapati utukufu yule Uliyemfanya adui.”

Maana yake ni kwamba ambaye ni adui wa Allaah hapati utukufu. Bali hali yake inakuwa ni udhalilifu, khasara na kufeli. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wakena Mtume Wakena Jibriylna Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.”[1]

Makafiri wote wako katika unyonge na wamedhalilishwa. Kwa ajili hiyo endapo waislamu wangehisi utukufu wa Uislamu, utukufu wa dini na utukufu wa ulinzi, basi makafiri hawa wasingelikuwa na hali hii ambayo wako nayo hivi sasa. Hali imefikia kiasi cha kwamba tunawatazama kwa mtazamo wa kificho. Tunawatazama kwa njia ya wao kutunyongesha na utukufu kwao. Kwa sababu kwa masikitiko makubwa waislamu wengi leo hawahisi utukufu kwa dini yao na wala hawakuchukua mafundisho ya dini. Badala yake wameegemea vitu vya kilimwengu na mapambo yake. Ndio maana wakapatwa na udhalilifu. Matokeo yake ndani ya nafsi zao makafiri ndio wakawa watukufu zaidi kuliko wao. Hata hivyo tunaamini kuwa makafiri ni maadui wa Allaah na kwamba Allaah amewaandikia udhalilifu kwa kila ambaye ni audi Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ

”Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, hao ndio katika waliodhalilishwa.”[2]

Hii ni khabari ya uhakika.

Kisha akasema:

كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ

”Allaah amekwishaandika kwamba bila shaka nitashinda Mimi na Mtume Wangu. Hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Aliyeshinda.”[3]

Kwa hiyo yeyote ambaye anamfanya Allaah kuwa uadui, basi ni dhalili na hawezi kabisa kuwa mtukufu. Isipokuwa kwa mtazamo wa ambaye haoni utukufu kwa njia nyingine isipokuwa kwa yaleyale aliyomo kafiri huyu. Ama kwa yule ambaye haoni kuwa utukufu unaweza kupatikana isipokuwa kwa kumfanya Allaah kuwa mpenzi (´Azza wa Jall) na kunyooka sawa na dini Yake, basi hawaoni watu hawa vyengine isipokuwa viumbe waliotwezwa zaidi na Allaah.

[1] 02:98

[2] 58:20

[3] 58:21

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 10/03/2024