12. Mawalii na wapenzi wa Allaah ni wale waumini na wenye kumcha

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema hali ya kuwa ni mwenye kuchota katika Aayah hii:

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

”Ambao wameamini na wakawa wanamcha.”[1]

”Ambaye ni muumini na mwenye kumcha Allaah ndiye walii wa Allaah.”

Amesema kweli (Rahimahu Allaah), kwa sababu hayo ndio ambayo yamefahamishwa na Qur-aan.

[1] 10:62-63

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 10/03/2024