Ni vipi yanafikiwa mapenzi na ulinzi (الولاية) wa Allaah? Yanafikiwa kwa sifa mbili ambazo Allaah amezibainisha ndani ya Kitabu Chake. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa wanamcha.”[1]

Sifa moja inahusiana na moyo na nyingine inahusiana na viungo vya mwili.

الَّذِينَ آمَنُوا

”Ambao wameamini… ”

Ni moyoni.

وَكَانُوا يَتَّقُونَ

”… na wakawa wanamcha.”[2]

Hii ni katika viungo vya mwili.

Wakati moyo na viungo vya mwili vinapotengemaa, basi mtu anapata mapenzi na ulinzi kwa sifa hizi mbili. Mawalii sio wale wanaojidai ambao wanafuata njia za watawa na Ahl-ul-Bid´ah ambao wanazusha ndani ya Shari´ah ya Allaah yale yasiyokuwemo na kujidai eti wao ndio mawalii. Kwa hivyo mapenzi ya Allaah (´Azza wa Jall) ambayo ndio yanamtukuza mtu yanapatikana kwa sifa hizi mbili:

1 – Imani.

2 – Kumcha Allaah.

[1] 10:62-63

[2] 10:62-63

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 10/03/2024