10. Kuomba utukufu kwa Allaah na akulinde na udhalilifu

Hakika hatwezeki yule Uliyemlinda na wala hapati utukufu yule Uliyemfanya adui – Hii ni kama sababu ya yale maneno yetu yaliyotangulia:

وتولنا فيمن توليت

”Uniangalie pamoja na wale Unaowaangalia.”

Allaah akimlinda mtu basi hamfedheheshi. Allaah akimfanyia uadui mtu basi hapati nguvu na utukufu. Maana ya haya ni kwamba tunatafuta utukufu kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) na tunajilinda kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na udhalilifu. Hawezi kudhalilika yeyote ambaye amelindwa na Allaah (Ta´ala). Cha muhimu ni kuhakikisha ulinzi huu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 10/03/2024