126. Masuala yanayohusiana na kuwaoza wanawake wa Kiislamu kwa makafiri

Katika hayo kuna masuala mengine vilevile:

Suala la kwanza: Kumuoza dada wa Kiislamu kwa kafiri. Haijuzu kumuozesha dada wa Kiislamu kwa kafiri. Ni mamoja kafiri huyo akiwa ni myahudi, mnaswara, mwabudu sanamu, mpagani au mkanamungu. Haijuzu kabisa kumuozesha dada wa Kiislamu kwa kafiri. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗأُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ

”Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina, japo akikupendezeni, na wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini. Mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina, japo akikupendezeni – hao [washirikina] wanaita katika Moto na Allaah Anaita katika Jannah na msamaha kwa idhini Yake.” (al-Baqarah 02:221)

Maneno Yake:

وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا

”Na wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini.”(al-Baqarah 02:221)

Bi maana mziwaozeshe dada waumini mpaka waamini kwanza. Akiacha ukafiri wake na akaingia katika Uislamu hapo ndipo inajuzu kumuozesha miongoni mwa dada wa Kiislamu. Amesema tena (Subhaanahu wa Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

”Enyi mlioamini! Wanapokujieni waumini wa kike waliohajiri, basi wajaribuni. Allaah anajua zaidi imani zao. Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.” (al-Mumtahinah 60:10)

Mtapojua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe kwa makafiri. Kwani yamekatika mafungamano yaliokuwa baina yao na ndoa kati ya dada wa Kiislamu na kafiri imevunjika. Kafiri haozeshwi dada wa Kiislamu mwanzoni kama ilivyo katika Aayah ya “al-Baqarah”:

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ

”Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.”

Na wala ndoa yao haitoendelea ikiwa dada huyo ataingia katika Uislamu na mume akawa ni kafiri, ndoa mwanamke huyo anatakiwa kutenganishwa naye:

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.”

Haijuzu kumuozesha kafiri mwanamke wa Kiislamu. Ni mamoja kuanza kumuozesha au wakaendelea kufanya hivo. Hili ni jambo ambalo wanachuoni wote wameafikiana juu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 163-164
  • Imechapishwa: 28/02/2019