125. Aina ya tano ya waislamu kuwafanya makafiri marafiki na vipenzi

5- Fungu la tano: Kuwapenda makafiri bila ya kuwasaidia dhidi ya waislamu. Hili kalikataza Allaah na linapingana na imani na akakanusha imani kwa yule mwenye kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُ مُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

”Kwa hakika mna kigezo chema kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale yote mnayoyaabudu badala ya Allaah. Tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya milele mpaka mumuamini Allaah pekee.” (al-Mumtahinah 60:04)

Suurat “al-Mumtahinah” yote inaharamisha kuwapenda makafiri hata kama watakuwa ni katika ndugu wakaribu kwa muislamu. Mwishowe akamalizia kwa kusema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ

”Enyi mlioamini! Msiwafanye wapenzi watu ambao Allaah amekasirika nao, wamekwishakata tamaa na Aakhirah kama walivyokwishakata tamaa makafiri kati ya watu wa makaburini.” (al-Mumtahinah 60:13)

Suurah “al-Mumtahinah” yote, kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake, inazungumzia maudhui ya kuwachukulia makafiri kama maadui na kutowapenda.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 160-162
  • Imechapishwa: 28/02/2019