125. Alikuwa ni muumini kwa mujibu wa Mtume

Nuuh al-Jaamiy´ (afk. 173), mwanachuoni wa Khuraasaan katika Fiqh.

155 – Haafidhw Ahmad bin Sa´d ad-Daarimiy amesema: Nimemsikia baba yangu akisema:

”Nimemsikia Abu Ismah Nuuh bin Abiy Maryam (Rahimahu Allaah) akiulizwa na bwana mmoja kama Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu ya mbingu. Akajibu kwa kusimulia Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati kijakazi alipomuuliza: “Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Juu ya mbingu.” Akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”[1]

Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad katika Kitaab-us-Sunnah” kutoka kwa Ahmad.

´Abbaad bin al-´Awwaam (afk. 185), mwanachuoni wa Waasitw katika Hadiyth.

156 – ´Abbaad bin al-´Awwaam amesema:

”Nilizungumza na Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake na kuona kuwa mwisho wa maneno yao wanachotaka kusema ni kwamba hakuna yeyote juu ya mbingu.  Naona kuwa wasiozeshwe na wala wasirithiwe.”[2]

[1] Nuuh ni mwenye kutuhumiwa kama ilivyokwishatangulia. Mtunzi ametaja masimulizi yake kutokana na elimu na uelewa wake, khaswa kwa kuzingatia kwamba yeye ni Hanafiy, na sio kwa sababu ya masimulizi na mapokezi yake. Ahmad bin Sa´iyd ad-Daarimiy ni katika waalimu wa al-Bukhaariy na Muslim. Sio yule ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy, mtunzi wa ”ar-Radd ´alaa al-Mariysiy” na ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, wala ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daarimiy, mtunzi wa ”al-Musnad”. Hata hivyo baba yake alikuwa ni Sa´iyd bin Swakhr ad-Daarimiy –  alikuwa si mwenye kutambulika kwa mujibu wa Abu Haatim katika ”al-Jarh wat-Ta´diyl” (2/1/34). Jina lake lilidondoka katika chapa iliyochapishwa ya ”as-Sunnah”, uk. 71.

[2] Ameipokea ´Abdullaah katika “as-Sunnah”, uk. 13 na 32, kupitia kwa Yahyaa bin Ismaa´iyl al-Waasitwiy, watu wengi wenye kuaminika wamepokea kutoka kwake pasi na yeye mwenyewe kufanywa kuwa mwenye kuaminika: Nimemsikia ´Abbaad bin al-´Awwaam pasi na jumla isemayo ”Naona kuwa wasiozeshwe na wala wasirithiwe”. Hata hivyo inapatikana katika ”as-Sunnah”, uk. 25, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, ambaye amesema:

”Hakuna wazushi ambao ni waovu zaidi kama wafuasi wa al-Jahm. Wanachotaka ni kusema kwamba hakuna yeyote juu ya mbingu. Naapa kwa Allaah! Naona kuwa wasiozeshwe wala kurithiwa.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 150-151
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy