Muhammad bin Ishaaq (afk. 150), kiongozi wa historia.

147 – Salamah bin al-Fadhwl amesema: ”Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia:

”Allaah (Ta´ala) yukama Alivyojisifu Mwenyewe. Kwani hakuna kilichokuwepo isipokuwa tu maji. Juu yake kuna ´Arshi. Juu ya ´Arshi yuko Mwenye utukufu na ukarimu. Yeye ni Mwenye kudhihiri katika ujuu Wake kwa njia ya kwamba Yuko juu ya viumbe Wake – hakuna chochote kilichopo juu Yake. Yeye Amefichikana katika uzungukaji Wake kwa viumbe Wake – hakuna chochote kilicho karibu kumliko. Yeye ni Mwenye kudumu asiyekuwa na mwisho. Kitu cha kwanza alichoumba ni nuru na giza. Kisha akazinyanyua mbingu saba kwa moshi. Kisha akazitandaza ardhi. Kisha akalingana juu ya mbingu, akazishikanisha na akakamilisha uumbaji wake ndani ya siku mbili. Akamaliza kuziumba mbingu na ardhi ndani ya siku sita. Halafu baada ya hapo akalingana juu ya ´Arshi.”[1]

Mis´ar bin Kidaam (afk. 153 au 155), mmoja katika maimamu.

148 – Yahyaa bin Ma´iyn amesimulia:

” Nilishuhudia wakati Zakariyyaa bin ´Adiy alipomuuliza Wakiy´ na kusema: ”Ee Abu Sufyaan, Hadiyth hizi kama mfano wa Hadiyth ya kwamba Kursiy ni mahali pa kuweka miguu miwili na mfano wake?” Akasema: ” ”Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, ath-Thawriy na Mis´ar bin Kidaam walikuwa wakizisimulia Hadiyth hizi na wala hawazifasiri chochote[2].”[3]

[1] Kuna unyonge kwa Salamah bin al-Fadhwl.

[2] Makusudio ni kwamba hawazipindishi maana kwa njia inayoenda kinyume na udhahiri wake.

[3] Mtunzi ameipokea kupitia kwa Yahyaa. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 145-146
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy