Kanuni inasema kwamba ni sharti ili mtu aweze kuingia katika Uislamu akubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ambayo maana yake ni mja kumpwekesha Allaah kwa matendo anayoyafanya kama vile anapoomba, anapoweka nadhiri, anaposwali, anapochinja, anaporukuu na aina nyinginezo za ´ibaadah.

Kwa kufupisha ni kwamba Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni kule kumpwekesha Allaah kwa matendo Yake (Subhaanah). Kuhusu Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ni mja kumpwekesha Allaah kwa matendo Yake. Kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah hakutoshelezi kumwingiza mtu katika Uislamu, kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa makafiri wa Quraysh. Kwa sababu hawakufanya kile kinachoipelekea; ambayo ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 05/03/2023