12. Sababu ya kumi na moja ya maisha mazuri: Moyo kuwa na nguvu na imara

11- Miongoni mwa tiba ambazo ni kubwa kwa viungo vya mioyo na bali pia viungo vya kiwiliwili ni moyo kuwa na nguvu na kutoyumbayumba na kuathirika na mawazo anayoyajenga mtu yanayozalisha fikira mbayambaya. Kwa sababu pale ambapo mtu atajisalimisha na kujengajenga mawazo na moyo wake ukayumbishwayumbishwa na mambo hayo katika khofu, maradhi na mengineyo, pia katika mambo ya kukasirisha, mambo ya kushawishi miongoni mwa mambo yanayoleta machungu, pia akawa anajengea picha ya kutokezewa na mambo mabaya na kuondokewa na yale mambo anayoyapenda, basi mambo hayo yanamwingiza katika misononeko na masikitiko na pia maradhi ya moyo na ya kiwiliwili na mporomoko wa viungo vyake, jambo ambalo lina athari mbaya ambalo watu wameshuhudia wenyewe madhara yake makubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 26
  • Imechapishwa: 17/06/2020