11. Sababu ya kumi ya maisha mazuri: Daima linganisha na hali mbaya zaidi

10- Miongoni mwa mambo yenye manufaa makubwa katika kuondosha masikitiko na msongo wa mawazo wakati anakuwa amefikwa na majanga ni yeye ajitahidi kuyawepesisha kwa kuyalinganisha na hali ambayo ni mbaya zaidi ambayo jambo linaweza kufikia na aitulize nafsi yake kwa jambo hilo. Atapofanya hivo basi afanye bidii katika kuwepesisha kiasi cha inavowezekana kuwepesisha. Kwa maandalizi na jitihada hizi zenye manufaa kunaondosha ile misononeko na masikitiko yake. Badala ya jambo hilo anakuwa ni mwenye kujitahidi kuleta manufaa na kuondosha madhara yanayoweza kuondoshwa.

Kunapotokea sababu za khofu, sababu za maradhi, sababu za ufakiri na kukosa vile vitu aina mbalimbali anavyokosa mtu, basi ayapokee hayo kwa utulivu na kuiandaa nafsi juu ya mambo hayo, bali hali mbaya zaidi inayoweza kufikia. Hakika kuiandaa nafsi katika kule kuyapokea mambo yenye kuchukiza kunawepesisha na kuondosha ile shida yake na khaswa pale atapoishughulisha nafsi yake kuyazuia kwa kiasi cha uwezo wake. Kwa hiyo juu yake kunakusanyika kuituliza nafsi pamoja na jitihada ambazo zinamshughulisha kutoyatilia umuhimu yale mambo yaliyomsibu. Sambamba na hilo anajibidisha kule kuileta upya nguvu yake katika kukabiliana na hayo mambo yenye kuchukiza na wakati huohuo katika jambo hilo anamtegemea Allaah na kuwa na uaminifu juu yake.

Hapana shaka kwamba mambo haya yana faida kubwa katika kufikia furaha na kukunjuka kwa kifua. Ukiongezea na zile thawabu zinazoandamana na mja duniani na Aakhirah. Haya ni mambo ambayo yameshuhudiwa na kujaribiwa. Uhalisia wake ni mwingi kutoka kwa wale waliyoyajaribu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 17/06/2020