10. Sababu ya tisa ya maisha mazuri: Kulazimiana na du´aa za Mtume

9- Miongoni mwa mambo yaliyo na manufaa makubwa katika yale mambo ya kuzingatia katika yale yanayokuja huko mbele ni kutumia du´aa hii ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba:

اللهم أصلح لي ديني الذي هو عصمة أمري، وأصلح لي دنياي التي فيها معاشي، وأصلح لي آخرتي التي إليها معادي، واجعل الحياة زيادة لي في كل خير، والموت راحة لي من كل شر

“Ee Allaah! Nitengenezee dini yangu ambayo ndio ngao ya jambo langu, nitengenezee dunia yangu ambayo humo ndio naishi, nitengenezee Aakhirah yangu ambayo ndio marejeo yangu, ufanye uhai wangu kuwa ni ziada kwangu juu ya kila kheri na ukifanye kifo kuwa ni mapumziko juu ya kila baya.”[1]

pia:

اللهم رحمتك أرجو فلا تكلني إلى نفسي طرفة عين، وأصلح لي شأني كله، لا إله إلا أنت

“Ee Allaah! Rehema Zako nazitarajia. Hivyo basi usinitegemezee nafsi yangu kiasi cha kupepesa kwa jicho, nitengenezee mambo yangu yote, hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe.”[2]

Mja atapolazimiana na du´aa hii ambayo ndani yake kuna kutengenezewa mambo ya dini na ya dunia kwa moyo wenye mazingatio, nia ya kweli pamoja na kupambana juu ya yale mambo yanayohakikisha jambo hilo, basi Allaah atamhakikishia yale aliyoomba, alichokitarajia na humfanyia. Badala yake misononeko yake hugeuka furaha.

[1] Muslim.

[2] Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 17/06/2020