12. Ni wakati gani Quraysh walijenga Ka´bah?

Swali 12: Ni wakati gani Quraysh walijenga Ka´bah?

Jibu: Quraysh walijenga Ka´bah wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na umri wa miaka 35. Wakamtaka ushauri aamue ni nani atakayeweka jiwe jeusi. Akaliweka kwenye kitambaa na akasema kila kabila lishike katika ncha ya kitambaa hicho. Yalikuwa makabila manne. Pindi walipolinyanyua hadi mahali pake na akaliweka mwenyewe mahali pake kwenye Ka´bah.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 94
  • Imechapishwa: 08/09/2023