12. Mwenye kukaa I´tikaaf kukaa kwenye paa la au koridoo ya msikiti

Swali 12: Inafaa kwa mwenye kukaa I´tikaaf katika msikiti Mtakatifu kutoka kwa ajili ya kula au kunywa? Inafaa kwake kukaa juu ya paa la msikiti kwa ajili ya kusikiliza darsa?

Jibu: Ndio, inafaa kwa ambaye kakaa I´tikaaf kwenye msikiti Mtakatifu au kwenginepo kutoka kwa ajili ya kula au kunywa ikiwa ameshindwa kukileta msikitini, kwa sababu hilo ni jambo lililomlazimu. Ni kama ambavo inafaa kwake kutoka kukidhi haja fulani. Pia atatakiwa kutoka kwenda kuoga janaba akiwa yuko na janaba.

Kuhusu kukaa juu ya paa la msikiti haidhuru. Kwa sababu kutoka kwenye mlango wa msikiti wa chini kupanda juu ya paa ni hatua chache tu. Isitoshe mtu huyu anakusudia pia kurejea msikitini. Hakuna neno kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 16
  • Imechapishwa: 12/04/2021