Swali 11: Mtu akamilishe swalah ya Tarawiyh usiku wa kuamkia ´iyd?

Jibu: Ukithibiti mwezi mwandamo usiku wa tarehe thelathini Ramadhaan basi haitakiwi kuswali swalah ya Tarawiyh wala kisimamo cha usiku. Hilo ni kwa sababu swalah ya Tarawiyh na kisimamo cha usiku inakuwa katika Ramadhaan. Kukithibiti kumalizika kwa mwezi basi hakuswaliwi. Watu wataondoka misikitini kwenda majumbani mwao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 15
  • Imechapishwa: 12/04/2021