10. Katika hali hii kuchotwa damu kuna hukumu moja kama kuumikwa

Swali 10: Uchotwaji wa damu nyingi unapelekea kumfunguza mfungaji?

Jibu: Uchotwaji wa damu nyingi ikiwa unapelekea katika yale yanayopelekea chuku katika kudhoofika kwa mwili na kuhitajia chakula basi hukumu yake ni kama ya kuumikwa. Ama ile damu inayomtoka mtu pasi na kutaka kwake, kwa mfano mtu akapatwa na jeraha na akavuja damu nyingi, ni kitu kisichodhuru. Kwa sababu ni pasi na kutaka kwa mtu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 15
  • Imechapishwa: 12/04/2021