Swali 13: Kuna kijana amejichua sehemu ya siri katika Ramadhaan hali ya kutokujua kuwa punyeto inafunguza na katika hali ambayo alizidiwa na matamanio yake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Hukumu yake ni kwamba hakuna kitu juu yake. Kwa sababu tulipitisha kutokana na yale yaliyotangulia kwamba mfungaji hafungui isipokuwa kwa sharti tatu:

1- Elimu.

2- Kukumbuka.

3- Matakwa.

Lakini nasema kuwa mtu analazimika kufanya subira kujizuia na punyeto kwa sababu ni haramu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

”Na wale ambao wanazihifadhi tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hivo, basi hao ndio wavukao mipaka.”[1]

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la barobaro! Yule atakayeweza miongoni mwenu kuoa basi na aoe. Hakika hilo linamfanya ainamishe macho na inahifadhi utupu wake. Yule asiyeweza basi ni juu yake afunge. Kwani kwake ni kinga.”[2]

Ingelikuwa inafaa kujichua sehemu ya siri basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelielekeza katika jambo hilo. Kwa sababu ndio jambo jepesi zaidi kwa mtu. Aidha mtu anahisi kustarehe tofauti na funga ambayo ina ugumu. Wakati Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoelekeza katika funga basi ikajulisha kuwa kitendo hicho hakifai.

[1] 23:05-07

[2] al-Bukhaariy (1905) na Muslim (3379).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 16
  • Imechapishwa: 12/04/2021