14. Ambaye haswali ni kama mfano wa myahudi na mnaswara

Swali 14: Ni ipi hukumu ya kufunga Ramadhaan na wakati huohuo mtu haswali?

Jibu: Ambaye anafunga na haswali haimfai kitu swawm yake, haikubaliwi kutoka kwake na haitakisiki dhimma yake. Bali hahitajii kufanya hivo muda wa kuwa haswali. Kwa sababu ambaye haswali ni kama mfano wa myahudi na mnaswara. Mnaonaje endapo myahudi au mnaswara atafunga na bado yuko katika dini yake atakubaliwa? Hapana. Kwa hivyo tunamwambia mtu huyu atubu kwa Allaah na aanze kuswali na kufunga. Allaah anamsamehe mwenye kutubu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 17
  • Imechapishwa: 15/04/2021