12. Kutenga kiasi fulani cha kisomo katika Tarawiyh

Swali: Ni yepi maoni yako – Allaah akuhifadhi na atunufaishe kwa elimu yako – kuhusu yale yanayofanywa na baadhi ya maimamu wanapotenga kiwango fulani cha Qur-aan juu ya kila Rak´ah na kila usiku?

Jibu: Sitambui chochote juu ya hilo. Kwa sababu jambo linarejea katika ile Ijtihaad ya imamu. Akiona ni katika manufaa kuzidisha katika baadhi ya nyusiku au baadhi ya Rak´ah kwa sababu ni mchangamfu zaidi, akajiona kuwa yuko na nguvu za kufanya hivo na akajiona kuwa ni mwenye kuburudika na kisomo na hivyo akazidisha baadhi ya Aayah ili yeye na wale walioko nyuma yake waweze kufaidika, akiifanya nzuri sauti yake na nafsi yake ikahisi vizuri kutokana na kile kisomo na akanyenyekea kwacho ananufaika yeye na wale walioko nyuma yake. Hatutambui ubaya wowote akizidisha baadhi ya Aayah katika baadhi ya Rak´ah au katika baadhi ya nyusiku. Wigo wake ni mpana na himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 10/04/2022