13. Ni ipi hukumu imamu kubeba msahafu?

Swali: Ni ipi hukumu imamu kubeba msahafu?

Jibu: Hakuna neno juu ya hili kutokana na maoni yenye nguvu zaidi. Wanazuoni wamekinzana juu ya hili. Lakini maoni sahihi zaidi ni kwamba hapana vibaya kusoma ndani ya msahafu ikiwa hakuhifadhi au hifdhi yake ikawa ni dhaifu ambapo akasoma ndani ya msahafu kwa ajili ya kuwanufaisha watu na kujinufaisha mwenyewe. Ni sawa kufanya hivo. al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) ametaja kwa cheni ya wapokezi pungufu katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba mtumwa wake aliyeachwa huru, Dhakwaan, alikuwa akimswalisha usiku kutoka ndani ya msahafu.

Kimsingi ni kwamba jambo hili linafaa. Athar ya ´Aaishah inalitilia nguvu jambo hili. Lakini kama ni wepesi kuhifadhi ndio bora zaidi. Kwa sababu jambo hilo linaukusanya moyo zaidi na kutikisika kwa uchache. Kubeba msahafu kunapelekea kuuweka chini, kuunyanyua na kutafuta zile kurasa wakati inapohitajika. Kwa hivyo akiepuka jambo hilo ndio bora.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 15
  • Imechapishwa: 10/04/2022