Swali: Niingiapo ndani ya swalah najihisi kuwa natokwa na upepo na wala sisikii kitu si sauti wala upepo, lakini ninapohisi hili huwa nikipuuza mpaka swalah inapomalizika. Ipi hukumu ya swalah yangu?

Jibu: Aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mtu ambaye anahisi kuwa ametokwa na kitu. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asitoke mpaka asikie ima sauti au upepo.”

Namna hii ndiyo alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika upokezi mwingine, kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atapohisi mmoja wenu kutokwa na kitu akatatizika ametokwa kweli na kitu au hapana, asiache swalah mpaka asikie ima sauti au upepo. Hivyo ni kuwa akitatizika ametokwa na kitu wudhuu´ wake haubatiliki wala swalah, swalah yake ni sahihi na wudhuu´ wake ni sahihi mpaka awe na uhakika kuwa ametokwa na kitu, ima kwa kusikia sauti au hewa. Au akitokwa na mkojo, twahara [wudhuu´] wake umebatilika na swalah. Lakini maadamu bado yuko na shaka tu swalah yake ni sahihi na wudhuu´ wake ni sahihi wala haibatiliki swalah yake. Kwa kuwa huu ni wasiwasi wa Shaytwaan na ni katika matendo yake khabithi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid= 8177
  • Imechapishwa: 10/04/2022