12. Kifunguzi cha kwanza cha swawm: kula na kunywa

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Ama baada ya hayo;

Miongoni mwa vitu vinavyofunguza na kumfanya mtu kuwa ni mwenye kufungua ni vifuatavyo:

1 – Kula na kunywa. Hapo ilikuwa ni baada ya alfajiri ya pili. Mwenye kula au akanywa kwa kutaka kwake mwenyewe hali ya kukumbuka kuwa amefunga, pasi na udhuru, basi swawm yake imeharibika. Mtu huyo anayo matishio makali. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

Analazimika kulipa siku hiyo pamoja na kuleta tawbah ya kweli, kujutia na kujikwamua.

[1] 02:187

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 34
  • Imechapishwa: 18/04/2023