54 – Muhammad bin Bashshaar ametukhabarisha: ´Abdul-Wahhaab ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:
”Baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna yeyote aliyevaa viatu, kupanda ngamia wa kike wala kupanda kipando aliye mbora kuliko Ja´far bin Abiy Twaalib.”[1]
55 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: Yaziyd bin Haaruun ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin ´Aamir ametukhabarisha:
”Alikuwa ´Umar anapomsalimia ´Abdullaah bin Ja´far, basi anasema: ”Amani ya Allaah iwe juu yako, ee mwana mwenye mabawa.”
56 – Muhammad bin Haatim bin Nu´aym ametukhabarisha: Muhammad bin ´Aliy amenikhabarisha: Baba yangu amenikhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Aswad bin Shaybaan, kutoka kwa Khaalid bin Shumayr, kutoka kwa ´Abdullaah bin Rabaah, kutoka kwa Abu Qataadah, ambaye ameeleza:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda mimbari na akamwamrisha mwenye kunadi aite: ”Swalah ya mkusanyiko!” Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Khabari mpya zimenifikia! Khabari mpya zimenifikia! Khabari mpya zimenifikia! Je, nisikuelezeni juu ya jeshi lenu linalopambana? Lilisonga mbele mpaka pale ambapo lilikutana na adui. Zayd akauliwa hali ya kuwa ni shahidi. Mwombeeni kwa Allaah msamaha. Kisha Ja´far akashika bendera na kuwashambulia vikali ambapo akauliwa hali ya kuwa ni shahidi. Mimi namshuhudilia kufa shahidi. Mwombeeni msamaha kwa Allaah. Kisha bendera ikachukuliwa na ´Abdullaah bin Rawaahah na akawa imara mpaka alipouliwa hali ya kuwa ni shahidi. Mwombeeni msamaha kwa Allaah. Kisha bendera ikachukuliwa na Khaalid bin al-Waliyd, ambaye hakuwa ni miongoni mwa viongozi.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanyanyua vidole vyake viwili na kusema: ”Ee Allaah, huu ni upanga miongoni mwa panga Zako. Fanya ushindi upatikane kupitia yeye!” Siku hiyo ndio Khaalid aliitwa upanga wa Allaah.”[2]
57 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Wahb bin Jariyr ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha: Nimemsikia Muhammad bin Abiy Ya´quub akisimulia kutoka kwa al-Hasan bin Sa´d, kutoka kwa ´Abdullaah bin Ja´far, aliyesema:
”Kwa muda wa siku tatu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisubiri familia ya Ja´far imjilie. Kisha ikamjilia na kusema: ”Msilie kwa ajili ya ndugu yangu baada ya siku ya leo.” Kisha akasema: ”Nileteeni wana wa ndugu yangu.” Akaletewa nao kana kwamba ni vifaranga. Akaamrisha wanyolewe vichwa vyao kisha akasema: ”Kuhusu Muhammad anafanana na ami yangu Abu Twaalib. Kuhusu ´Abdullaah, anafanana na umbile na tabia yangu.” Kisha akanishika mkono wangu na kusema: ”Ee Allaah! Mfanye Ja´far ashike mahali pa familia yake baada yake na ibariki biashara ya ´Abdullaah. Ee Allaah! Mfanye Ja´far ashike mahali pa familia yake baada yake na ibariki biashara ya ´Abdullaah.”[3]
[1] at-Tirmidhiy (3764), aliyesema Hadiyth ni nzuri, Swahiyh na geni. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Mu´allimiy katika “al-Anwaar al-Kaashifah”, uk. 149.
[2] Ahmad (5/299, 300 na 301). Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir.
[3] Ahmad (1/204-205). Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir.
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 58-60
- Imechapishwa: 07/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 58-60
Imechapishwa: 07/09/2026
https://firqatunnajia.com/12-fadhilah-za-jafar-bin-abiy-twaalib/