52 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: Yaziyd ametukhabarisha: al-´Awwaam ametukhabarisha: Sa´iyd bin Jamhaan amenihadithia, kutoka kwa Safiynah, mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ukhaliyfah baada yangu utakuwa kwa miaka thelathini. Kisha baada ya hapo itakuwa ni utawala wa ufalme.”
Tukahesabu na tukafikia kwa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy[1].
53 – ´Abdah bin ´Abdillaah na al-Qaasim bin Zakariyyaa wametukhabarisha, kutoka kwa Husayn, kutoka kwa Zaa-idah, kutoka kwa Husayn bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa al-Hurr bin Swayyaah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Akhnas, kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd, aliyesema:
”Hiraa´ ilitikisika, ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Tulia, ee Hiraa´! Hakuna aliye juu yako isipokuwa Nabii, mkweli au shahidi.”
Juu yake alikuwa amesimama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d bin Abiy Waqqaas na mimi[2].
[1] Abu Daawuud (4646) na at-Tirmidhiy (2226). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3257).
[2] Abu Daawuud (4648) na at-Tirmidhiy (3757). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (134).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 56-57
- Imechapishwa: 07/09/2026
52 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: Yaziyd ametukhabarisha: al-´Awwaam ametukhabarisha: Sa´iyd bin Jamhaan amenihadithia, kutoka kwa Safiynah, mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ukhaliyfah baada yangu utakuwa kwa miaka thelathini. Kisha baada ya hapo itakuwa ni utawala wa ufalme.”
Tukahesabu na tukafikia kwa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy[1].
53 – ´Abdah bin ´Abdillaah na al-Qaasim bin Zakariyyaa wametukhabarisha, kutoka kwa Husayn, kutoka kwa Zaa-idah, kutoka kwa Husayn bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa al-Hurr bin Swayyaah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Akhnas, kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd, aliyesema:
”Hiraa´ ilitikisika, ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Tulia, ee Hiraa´! Hakuna aliye juu yako isipokuwa Nabii, mkweli au shahidi.”
Juu yake alikuwa amesimama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d bin Abiy Waqqaas na mimi[2].
[1] Abu Daawuud (4646) na at-Tirmidhiy (2226). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3257).
[2] Abu Daawuud (4648) na at-Tirmidhiy (3757). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (134).
Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 56-57
Imechapishwa: 07/09/2026
https://firqatunnajia.com/11-fadhilah-za-abu-bakr-umar-uthmaan-na-aliy/