46 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ya´quub bin Abiy Haazim ametukhabarisha: Sahl bin Sa´d ametukhabarisha  kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema siku ya Khaybar:

“Kuna mtu nitampa bendera kesho asubuhi ambaye Allaah atafungua mji kwa mikono yake. Ni mtu anampenda Allaah na Mtume Wake na Allaah na Mtume Wake wanampenda.” Ilipofika asubuhi watu wakarauka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kila mmoja akitaraji kupewa nayo. Ndipo akasema: “Yuko wapi ´Aliy bin Abiy Twaalib?” Wakasema: “Ni mgonjwa wa macho, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: ”Aletwe kwangu.” Akaletewa naye, ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtemea mate machoni mwake na kumuombea du´aa. Akapona papohapo kana kwamba hakuwa mgonjwa. Akampa bemdera. ´Aliy akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Niwapige vita mpaka wawe kama sisi?” Akasema:  “Nenda zako taratibu na kwa upole mpaka ufike maeneo yao. Naapa kwa Allaah! Lau Allaah atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”[1]

47 – al-´Abbaas bin ´Abdil-´Adhwiym ametukhabarisha: ´Umar bin ´Abdil-Wahhaab ametuhadithia: Mu´tamir bin Sulaymaan ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Rib´iy, kutoka kwa ´Imraan bin Huswayn, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nitampenda bendera mtu ambaye anampenda Allaah na Mtume Wake – au alisema: ”… Allaah na Mtume Wake wanampenda.” Akamwita ´Aliy ambaye alikuwa anaumwa macho. Allaah akafungua mji kupitia mikononi mwake.”

Bi maana ´Aliy.

48 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: Ya´laa bin ´Ubayd ametuhadithia: Yaziyd bin Kaysaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Leo nitampenda bendera mtu ambaye anampenda Allaah na Mtume Wake na Allaah na Mtume Wake wanampenda.” Watu wakaanza kupeleleza, ambapo akasema: ”Yuko wapi ´Aliy?” Wakasema: “Ni mgonjwa wa macho.” Akamwita. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatema mate viganjani mwake kisha akamfuta kwavyo macho ya ´Aliy. Halafu akampa bendera. Siku hiyo Allaah akaufungua mji kupitia kwake.”

. Akapona papohapo kana kwamba hakuwa mgonjwa. Akampa bendera.

49 – Nilimsomea Muhammad bin Sulaymaan, kutoka kwa Ibn ´Uyaynah, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Abu Ja´far Muhammad bin ´Aliy, kutoka kwa Ibraahiym bin Sa´d bin Abiy Waqqaas, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia:

”Tulikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati ambapo palikuwepo na watu waliokaa pale. Wakati ´Aliy alipoingia ndani, wakalaumiana wao kwa wao na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Haina maana kwamba ametutowa sisi na kumwingiza ndani yeye.” Hivyo    wakaamua kurudi. Wakati waliporudi akasema: ”Naapa kwa Allaah! Haikuwa mimi niliyemwingiza ndani na kukutoeni nje; ilikuwa ni Allaah ndiye kamwingiza ndani na kukutoeni nje.”[2]

50 – Muhammad bin al-´Alaa’ ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametuhadthia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa ´Adiy bin Thaabit, kutoka kwa Zirr bin Hubaysh, kutoka kwa ´Aliy, aliyesema:

”Naapa kwa Yule ambaye amepasua mbegu na akaumba nafsi! Mtume asiyejua kuandika wala kusoma alinizungumza kwamba hakuna atakayenipenda mimi isipokuwa muumini na wala hakuna atakayenichukua mimi isipokuwa mnafiki.”[3]

51 – Ahmad bin Maniy´ alitusomea, kutoka kwa Hushaym, kutoka kwa Abu Haashim, kutoka kwa Abu Mijliz, kutoka kwa Qays bin ´Abbaad, ambaye amesema:

”Nilimsikia Abu Dharr akiapa kwamba Aayah hii[4] iliteremshwa kuhusiana na wale waliopigana siku ya Badr; Hamzah, ´Aliy, ´Ubaydah bin al-Haarith, ´Utbah bin Rabiy´ah, Shaybah bin Rabiy´ah na al-Waliyd bin ´Utbah.”[5]

[1] al-Bukhaariy (309) na Muslim (405).

[2] Dhaifu kwa mujibu wa al-Khatwiyb al-Baghdaadiy katika “Taariykh Baghdaad” (2/293-294).

[3] Muslim (131).

[4] Allaah (Ta´ala) amesema:

هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ

”Hawa ni wapinzani wawili wanabishana juu ya Mola wao.” (22:19)

[5] al-Bukhaariy (3969).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 54-56
  • Imechapishwa: 07/09/2026