41 – Muhammad bin al-´Alaa’ ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametukhabarisha: al-A´mash ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa Ibn Buraydah, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yule ambaye mimi ndiye mpenzi wangu, basi ´Aliy pia ni mpenzi wake.”[1]
42 – Abu Daawuud Sulaymaan bin Sayf ametukhabarisha: Abu Nu´aym ametuhadithia: ´Abdul-Malik bin Abiy Ghaniymah ametukhabarisha: al-Hakam ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa Buraydah, ambaye amesema:
”Tulitoka pamoja na ´Aliy kwenda Yemen. Nikaona ususuwavu kutoka kwake, ambapo nikamtajia jambo hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nikamdogesha ´Aliy. Uso wake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukawa unabadilika. Akasema: ”Ee Buraydah! Je, mimi si nina haki zaidi kwa waumini kuliko wao wenyewe?” Nikasema: ”Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Ndipo akasema: ”Yule ambaye mimi ndiye mpenzi wangu, basi ´Aliy pia ni mpenzi wake.”
43 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ja´far – Ibn Sulaymaan – ametukhabarisha, kutoka kwa Yaziyd ar-Rishk, kutoka kwa Mutwarrif bin ´Abdillaah, kutoka kwa ´Imraan bin Husayn, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika ´Aliy anatokana nami nami natokana naye. Naye ni walii wa kila muumini anayekuja baada yangu.”[2]
44 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: Yahyaa bin Abiy Aadam ametukhabarisha: Israa’iyl ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Ishaaq: Hubshiy bin Junaadah as-Saluuliy amenihadithia:
”´Aliy anaotokana nami nami natokana naye. Hatofikisha kutoka kwangu isipokuwa mimi mwenyewe au ´Aliy.”[3]
45 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Yahyaa bin Hammaad ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan: Habiyb bin Abiy Thaabit ametuhadithia, kutoka kwa Abut-Twufayl, kutoka kwa Zayd bin Arqam, ambaye amesema:
”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliporejea kutoka katika hijja ya kuaga, alipiga kambi Ghadiyr-ul-Khumm. Aliamrisha kupandishwa juu mwavuli na kukasafishwa. Kisha akasema: ”Kana kwamba nimeitwa na kuitikia. Nimekuachieni vizito viwili ambavyo kimoja wapo ni kikubwa zaidi kuliko kingine: Kitabu cha Allaah na familia yangu. Hivyo basi tazameni ni namna gani mtavyokabiliana navyo baada yangu. Kwani hakika havitoachana mpaka virudi kwangu kwenye Hodhi.” Kisha akasema: ”Allaah ndiye walii wangu nami ni walii wa kila muumini.” Kisha akashika mkono wa ´Aliy na kusema: ”Yule ambaye mimi ndiye mpenzi wangu, basi huyu pia ni walii wake. Ee Allaah! Mpende yule mwenye kumpenda na mfanye adui yule mwenye kumfanya adui.” Nikamwambia Zayd: ”Umeyasikia hayo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: ”Hapakuwepo yeyote chini ya mwavuli isipokuwa alimuona kwa macho yake na akayasikia kwa masikio yake.”
[1] Ahmad (5/347, 350 na 361) na al-Haakim (3/110).
[2] at-Tirmidhiy (3712), ambaye amesema ni nzuri na geni. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3712).
[3] at-Tirmidhiy (3719), ambaye amesema ni nzuri, Swahiyh na geni. Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3719).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 51-54
- Imechapishwa: 07/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 51-54
Imechapishwa: 07/09/2026
https://firqatunnajia.com/09-aliy-anatokana-na-mtume-na-mtume-anatokana-na-aliy/