12. Daraja ya pili ya makadirio: Kuandika

Daraja ya pili: Kuandika. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ameyaandika makadirio yote katika ubao Uliohifadhiwa. Daraja zote hizi mbili Allaah (Ta´ala) amezitaja katika Aayah pale aliposema:

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚإِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[1]

Allaah (Subhaanah) ameanza kwa elimu na kusema:

إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Hakika hayo yamo katika Kitabu.” (22:70)

Bi maana yameandikwa kwenye ubao Uliohifadhiwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika.” Ikasema: “Mola! Niandike nini?” Akasema: “Andika yatayokuwa mpaka siku ya Qiyaamah.”

Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kama matendo yetu yameshakadiriwa au bado akasema kuwa yameshakadiriwa. Pindi alipoulizwa tena matendo yana maana gani na kama mtu si ategemee makadirio akasema:

“Tendeni! Kila mmoja amesahilishiwa kwa kile alichoumbiwa kwacho.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamrisha kutenda. Hivyo tenda! Hakika wewe umesahilishiwa kwa kile ulichoumbiwa kwacho. Baada ya hapo akasoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno Yake (Ta´ala):

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ

“Basi yule anayetoa [katika mali zake] na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi [kufuata maamrisho ya dini]. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza [kwa kuwa ni tajiri] na akakadhibisha lililo jema zaidi, Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[2]

[1] 22:70

[2] 92:05-10

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/223-224)
  • Imechapishwa: 25/10/2016