11. Daraja ya kwanza ya makadirio: Elimu

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa makadirio na mipango ina daraja nne:

Ya kwanza: Elimu. Mwanaadamu anatakiwa kuyakinisha kuwa Allaah (Ta´ala) juu ya kila kitu ni mjuzi na kwamba anajua yote yaliyomo mbinguni na ardhini. Haijalishi kitu ikiwa inahusiana na matendo yake mwenyewe au matendo ya waja Wake. Mtu anatakiwa kutambua kuwa hakuna kitu mbinguni wala ardhini ambacho kinafichikana kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/223)
  • Imechapishwa: 25/10/2016