10. Utashi wa Allaah ni wenye kuafikiana na hekima Yake

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwa mwanaadamu anatenda na anazungumza kwa khiyari na wakati huo huo uwezo na utashi wake ni wenye kunyenyekea utashi wa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini vilevile kuwa utashi wa Allaah (Ta´ala) unaafikiana na hekima Yake na kwamba utashi Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) haukuachiwa hivihivi. Utashi Wake ni wenye kuafikiana na hekima Yake. Moja katika majina ya Allaah (Ta´ala) ni Mwenye hekima, al-Hakiym, ambaye kwa umairi mkubwa anayahukumu mambo kilimwengu, Kishari´ah na kimatendo. Kwa hekima Yake Allaah (Ta´ala) anamkadiria ni nani atayeongozwa katika waja ambaye Anajua kuwa anataka haki na ana moyo mwema na ni nani atayepotezwa katika waja ambaye anajua kuwa haukubali Uislamu. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anakataa huyu kuwa katika wenye kuongozwa maadamu Allaah hajajadidi na kubadilisha utashi Wake. Allaah (Ta´ala) juu ya kila jambo ni muweza. Allaah anakataa mambo kupitika pasi na sababu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/222-223)
  • Imechapishwa: 25/10/2016