111. Upambanuzi juu ya tuhuma kwamba Ibn ´Abdil-Wahhaab anamkufurisha anayeapa kwa asiyekuwa Allaah

Maneno yake:

“Isitoshe kwamba eti nakemea kutembelea makaburi ya wazazi wake wawili na wengineo.”

Haya yanatokana na yale waliyosema kwamba anawakufurisha wale waliomtangulia. Eti yeye anawaambia watu wasiwatembelee wazazi wao kwa sababu ni makafiri. Huku ni kumsemea uongo. Shaykh hajui kuhusu wale waliokufa na wamekufa katika hali gani. Kimsingi ni kwamba wafu wa waislamu wanadhaniwa vyema. Huku ni kumsemea uongo Shaykh (Rahimahu Allaah).

Maneno yake:

“Aidha kwamba namkufurisha wenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kuapa kwa asiyekuwa Allaah:

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru au ameshirikisha.”[1]

Lakini haina maana kwamba ni ukafiri unaomtoa mtu nje ya Uislamu. Inahusiana na ukafiri mdogo. Shirki ndogo haimtoi mtu nje ya dini. Ambaye anasema kuwa ni kufuru au ni shirki, ikiwa anakusudia kwamba ni shirki ndogo au kufuru ndogo, ni sahihi. Kwa sababu Mtume ameita kuwa ni kufuru na kwamba ni shirki. Lakini akiwa anakusudia kwamba ni kufuru inayomtoa mtu nje ya dini ni jambo batili.

[1] Abu Daawuud (3251), at-Tirmidhiy (1535) na Ahmad (02/125 nambari. 6072).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 154
  • Imechapishwa: 08/06/2021